Habari

Hizi ni faida za kununua ama kuuza bidhaa mtandaoni (online classified ads)

Unapozungumzia kuhimiza ukuaji wa biashara za mfumo wa kisasa, hakuna njia nzuri na ya bei rahisi kama matangazo ya aina mbalimbali ya mtandaoni (online classified advertisements).

olx-nigeria

Hii si kwasababu tu kwakuwa ni njia rahisi ya kupanua ufikiwaji wa masoko mapya na fursa, lakini pia ni nafuu mno kuweza kuwavutia wateja wa baadaye. Miongoni mwa faida kubwa ya matangazo hayo yaani ‘Online Classified Ads’ ni kwamba yanaweza kufungua fursa zisizohabika kwa wauzaji na biashara zinazofanana licha ya kuwasaidia kuwafikia wengine ndani ya sekunde chache tu.

Kama haitoshi, mchakato wote wa kuweka matangazo hayo ni rahisi na hautumia nguvu wala muda mwingine.

Mfano mzuri ni mtandao wa OLX Nigeria ambao ni sehemu ya matawi mengi ya OLX.

Katika mtandao huo watu wanaweza kuuza vifaa vyao kama simu, laptop, TV na vingine ambavyo hawavihitaji tena na mtu mwingine ambaye anahitaji vitu hivyo kununua kupitia mtandao huo. Mitandao hiyo ya aina a OLX inawakutanisha wauzaji na wanunuzi wengi kwa wakati mmoja kwa njia ya mtandao peke yake.

Faida nyingine ya matangazo hayo kuwa yanaweza kufikiwa na mamilioni ya wateja wa uhakika na nafasi ya kuonekana ni kubwa. Kuweka tangazo lako mtandaoni si kwamba ni bure tu bali pia husaidia kuokoa muda, fedha na jitihada kwakuwa matangazo ya internet yanaweza kuweka na kubadilishwa muda wowote. Huhitaji kusubiri mpaka mtu mwingine akuwekee, kazi unaifanya mwenyewe.

Zaidi ni kuwa watangazaji wanaweza kuongeza pia mawasiliano yao (kama vile namba za simu, jina la website, anuani ya biashara na vingine) ili wateja waliovutiwa waweze kuuliza na kukusanya taarifa nyingi kadri iwezekanavyo kabla ya kuchukua uamuzi wa kununua bidhaa husika.

Faida zote hizi ni muhimu kwa wauzaji hasa wale ambao hawana mtaji mkubwa wa kufanya matangazo ya gharama kubwa kutangaza biashara zao. Matangazo ya reja reja yanaweza kutumika pia kuongeza uonekaji zaidi wa kurasa za website za biashara husika kwenye search engine kama Google na Bing.

Kingine ni kuwa matangazo haya ya bure yanaweza kufanywa na makundi ya watu wote bila kuzingatia mahali ama nyanya fulani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents