Burudani

Hizi ni chati za Afrika ambazo ‘Never Ever’ ya Vanessa Mdee inasumbua kwa sasa

Wimbo wa Vanessa Mdee ‘Never Ever’ ambao video yake ilianza kutoka October 9 kwa kutambulishwa kupitia Trace Urban na kufatiwa na audio iliyotoka Oct 12, unaendelea kushika chati mbalimbali za vituo vya TV pamoja na radio barani Afrika.

vee4

Baadhi ya chati ambazo wimbo huo uliopikwa na producer anayesumbua sana kwa sasa Nahreel wa The Industry na video kuongozwa na Justin Campos, ni pamoja na Africa Top 10 ya Trace Urban ambapo kwa wiki hii imekamata nafasi ya pili.

Chati nyingine ni Africa Top 10 ya Nigezie TV ya Nigeria ambapo iko nafasi ya tatu.

‘Never Ever’ pia iko nafasi ya nne kwenye chati ya kituo cha radio cha Afrika Kusini, YFM

Kwenye chati ya NAIJA 102.7 FM IB ya Nigeria iko namba moja.

Kwenye African Count Down ya Crooze Fm ya Uganda iko nafasi ya nne

Kwenye African Top 10 ya The Beat Fm ya Nigeria iko nafasi ya kwanza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents