Michezo

Hispania ya watoa hofu Madaktari wa Chelsea kuhusu hali ya Diego Costa

Mshambualiaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa ameambiwa hali yake si mbaya baada ya kuumia akiwa kwenye timu ya taifa ya Hispania.

Cost ambaye anamiaka 28, alilazimika kuondoka kwenye uwanja wa mazoezi mapema Jumapili baada ya kupata majeraha ya mguu na kifundo cha mguu.

Taarifa iliyosomeka kwenye, Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) limethibitisha: “Diego Costa alilazimika kuondoka mazoezini kufuatia majeraha ya mguu na kifundo cha mguu, ambayo yamemlazimu kufanyiwa vipimo kadhaa (X-ray na TAC) katika Kliniki ya Sanitas iliyoko La Moraleja, ambako aliambiwa safi.

“Mwanasoka huyo bado yupo chini ya uangalizi na ataendelea kubaki na timu katika kambi ya mazoezi.

“Madaktari wa Chelsea FC wamejulishwa kuhusu hali ya mchezaji.”

Costa anatarajiwa kucheza kwenye kikosi cha Hispania kitakachoikabili Ufaransa mechi ya kirafiki mjini Paris siku ya leo Jumanne usiku.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents