Michezo

Hiki ndicho kikosi cha Yanga kitakachoanza kwenye mechi yake ya leo dhidi ya Madeama SC

Timu ya Yanga imekitaja kikosi chake kitakachoanza leo kwenye mechi yake dhidi ya wenyeji wao Madeama SC ya Ghana kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

yanga-vs-medeama_1jbj2prvw2n814jyxmrvr5964

Julai 16 mwaka huu timu hizo zilikutana kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam walitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.

Timu ya Yanga inatakiwa ishinde kwenye mechi hiyo ili ijiweke kwenye mazingira mazuri ya kuwania nafasi mbili za kufuzu kwenye kundi lake ikiwa kwa sasa inaburuza mkia ikiwa na pointi moja na Tp Mazembe ndiyo wanaongoza kundi hilo wakiwa na point saba.

Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewataja wachezaji 11 watakaoanza kwenyemechi hiyo akiwemo Deogratius Munish, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Mbuyu Twite, Saimon Msuva, Thaban Kamusoko, Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.

Wachezaji wa akiba ni pamoja na Ally Mustafa, Vicent Andrew, Said Juma, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi, Amissi Tambwe na Malimi Busungu. Kila la kheri kwa timu ya Yanga kwa kuwa wao ndiyo wawakilishi pekee kutoka Tanzania kwenye mashindano hayo makubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents