Burudani

Watu wanadhani nimepagawa – Hawa wa ‘Nitarejea’ ya Diamond

Msanii ambaye aliwahi kufanya collabo na Diamond ‘Nitarejea’, amesema wakati mwingine watu wanadhani amepagawa, kitu ambacho si kweli na kwamba kwa anatafuta menejimenti itakayosimamia kazi zake.

duuu

Siku za nyuma Hawa alikumbwa na matatizo kadhaa baada ya kutelekezwa na mwanaume aliyempatia ujauzito na pia aliwahi kupatwa na skendo za matumizi ya madawa ya kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Hawa alisema: “Sasa hivi naogopa watu, nahitaji mtu wa kunisimamia, nahitaji kabisa mtu wa kunisimamia niweze kufanya vitu vyangu. Lakini siwezi kujieleza yaani , nikijieleza kwa kila mtu siwezi kumaliza, mtu mwenye imani yake anaweza akanisaidia, lakini siwezi kusema kwa kila mtu naonekana mi mwendawazimu, naonekana kama nimepagawa saa nyingine.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents