Burudani

Hii ni aina nyingine ya muziki anaoweza kuufanya Msami

Kama umekua mfuatiliaji wa muziki wa msanii Msami kuanzia kwenye kazi zake za mwanzo mpaka za hivi karibuni, lazima umegundua kuwa ni mtu anaYependa sana kufanya muziki wa Afro.

Msanii huyo ameweka wazi aina nyingine ya muziki anaYoweza kuifanya mbali na watu walivyomzoea.

“Naweza kufanya rnb kidogo, naweza kufanya dancehall, lakini naweza kurap pia,” Msami aliniambia kwenye mahojiano yangu kupitia Kings FM.

Bila shaka mashabiki wa muziki wana hamu kubwa ya kusikia ladha ya tofauti kutoka kwa mkali huyo wa Step by Step ambaye ni zao la Jumba la Vipaji Bongo, THT.

Imeandikwa na Prince Ramalove (Kings FM).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents