Habari

Hii ndiyo faida iliyoipata kampuni ya Facebook kwenye robo ya mwaka jana

Kampuni ya mtandao wa Facebook bado inazidi kujiingiza fedha za kutosha – Imetoa ripoti yake ya faida walioipata katika robo ya kwanza ya mwaka 2016.

Katika ripoti hiyo Facebook imetangaza kuingiza faida ya dola bilioni 3.49 na kuzidi makadirio yao waliojiwekea huku hisa zake zikipanda thamani kwa asilimia 2 baada ya biashara ya saa moja. Mapema mwezi April mwaka jana kampuni hiyo ilitoa ripoti ya kuongezeka kwa mapato yake kutoka dola milioni 512 kwa mwaka juzi hadi mapato ya dola bilioni 1.5 kuanzia mwezi Januari na Machi mwaka 2016.

Wakati huo huo mahakama moja ya kijimbo nchini Marekani imeitaka Facebook kuilipa dola milioni 500 kampuni ya ZeniMax Media (inachapisha video games) ili iweze kuzindua Virtual Reality Headset.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents