Michezo

Hii ndio Yanga! Milango ya uwanja wa taifa yafungwa

Mechi ya Yanga na Tp Mazembe leo imevunja rekodi baada ya watu kujaa zaidi hali iliyopelekea milango ya Uwanja wa taifa kufungwa mapema.

chemical-kama-ipo

Yakiwa yamebakia takriban masaa matatu kuanza kwa mechi ya kombe la shirikisho kati ya Yanga na Tp Mazembe, vikosi vya usalama vimeamuru milango ya uwanja wa taifa kufungwa mapema kutokana na uwanja huo kujaa huku watu wengine wazuiwa kubaki nje.

Uongozi wa Yanga kupitia kwa mwenyekiti wake, Yusuph Manji ulitangaza kununua tiketi zote za mechi hiyo na kuwagawia mashabiki kwa kwenda kutazama mechi hiyo bure.

Hali hiyo iliyotokea leo inaweza ikawa imeweka rekodi kwenye soka hapa Bongo kutokana na watu kuanza kufika mapema zaidi uwanjani na machache baadae uwanja huo umeonekana kujaa kupita kiasi mpaka milango KUfungwa.

IMG-20160628-WA0014

Timu ya Yanga inatakiwa kupata ushindi mechi ya leo ili iweze kujihakikishia nafasi nzuri kwenye kundi lao litakaloweza kutoa timu mbili pekee zitakazosonga mbele. Mpaka sasa timu hiyo inashika nafasi ya tatu haku kundi hilo likiongozwa na timu TP Mazembe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents