Burudani

Hii ndio maana ya jina la wimbo ‘Ya Kulevya’ wa Weusi

‘Ya Kulevya’ ni moja kati ya majina ya nyimbo zilizowashtua mashabiki hasa katika kipindi hiki tulichopo sasa. Weusi wamefunguka maana ya jina la wimbo huo.

Akiongea kwa niaba ya wasanii wa kundi hilo, Nick wa Pili amekiambia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, wimbo huo unamuhusu baba anayependwa kwenye familia yake lakini baada ya muda upendo huo unamlevya na kuanza kufanya vitu vya tofauti.

“Inamzungumzia baba wa familia kama kiongozi aliyepewa dhamana ya kuiongoza familia, mama na familia imempenda sana baba. Kawaida ya baba akipendwa anachukulia poa, upendo umemlevya baba anaanza kufanya mambo yasiyofaa, anakuwa mtu wa ‘totoz’, Kiki,” amesema Nick.

“Msanii ni zao la mazingira yake tumetumia maneno yanayozunguka sasa hivi tumeyatoa kwenye ‘muktadha’ yake tumeyaleta kwenye wimbo wetu tukatoa kitu,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents