Burudani

Hi Nicki!! Iggy Azalea apata shavu kwenye Fast and Furious 7

Iggy Azalea anazidi kufanikiwa. Kutoka kwenye ‘Fancy’ na sasa kwenye filamu ya ‘Fast & Furious.

iggy

Rapper huyo wa Australia ataonekana pamoja Vin Diesel kwenye Fast & Furious 7. Kwenye filamu iliyopita ya Fast and Furious, Rita Ora alipewa shavu la kuonekana. Habari hiyo imetangazwa na Vin Diesel wakati akijibu swali kwenye interview aliyofanyiwa na Skyrock FM.

Fast & Furious 7 inatarajiwa kuingia sokoni April 3, 2015 ikiwa na waigizaji kama Ludacris, Tyrese, Dwayne Johnson, Michelle Rodriguez na marehemu Paul Walker.

Pamoja na hivyo, Iggy alichaguliwa kuwa mtangazaji wa show ya MTV, “House of Style,” itakayoanza kuoneshwa August 4 kupitia MTV.com. Hivi karibuni pia alitajwa kuwania vipengele 7 MTV Video Music Awards.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents