Burudani

‘Hercules’ ya The Rock yazidiwa nguvu na ‘Lucy’ ya Scarlett Johansson kwenye box office

Filamu ya Scarlett Johansson,’Lucy’ imeizidi filamu mpya ya Dwayne Johnson aka The Rock ‘Hercules’ kwa kuingiza dola milioni 44 weekend hii.

Hercules imeingiza dola milioni 29 na kufuatiwa na ‘Dawn of the Planet of the Apes’ iliyoshika nafasi ya tatu kwa kuingiza dola milioni 16.4.

Lucy filamu iliyoandikwa, kuongozwa na kutayarishwa Luc Besson na inayomhusu mwanamke anayepata nguvu za ajabu katika ubongo wake baada ya kidonge kuwekwa mwilini mwake, imevuka matazamio ya wachambuzi wa filamu na ilizidi gharama za utayarishaji wake katika siku tatu za kwanza tangu iingie sokoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents