BurudaniVideos

Haya ni maoni ya Lulu kuhusu Darassa, FA, Mavoko, Ommy Dimpoz, Ben Pol, Joh Makini, Nick wa Pili na ngoma zao

Elizabeth ‘Lulu’ Michael, ni shabiki mkubwa wa muziki.

Wiki iliyopita, muigizaji huyo alihost show ya Ngaz Kwa Ngaz ya EATV na kucheza video za nyimbo 20 za mwaka jana anazozikubali. Alikuwa na maoni mbalimbali kuhusu nyimbo hizo.

Kuhusu Dume Suruali wa Mwana FA f/ Vanessa Mdee

Alisema Vanessa Mdee alikuwa mtu sahihi kushirikishwa kwenye Dume Suruali

Alisema kama video ya Dume Suruali ingefanyika kwenye mazingira ya Tanzania ingepata story nyingi na ingekuwa bora

Kuhusu Moyo Mashine wa Ben Pol

Alisema alishangaa kubaini kuwa Moyo Mashine uliandikwa na muimbaji wa gospel Godluck Gosbert

Alisema video ya Moyo Mashine hajawahi kuielewa

‘Ben Pol ni mmoja wapo wa wasanii ambao inabidi tujivunie’

Kuhusu Perfect Combo wa Joh Makini f/ Chidinma

Alisema anampenda Chidinma na watu husema kuna namna wanafanana

Alidai Joh Makini na Chidinma wameingiza msemo mpya mjini ‘Perfect Combo’

Kuhusu Lover Boy wa Barnaba

Alisema hakufikiria kama video ya wimbo Lover Boy ilifanyika Bongo

‘ Dread za Barnaba zimekuwa vizuri, smart zimekuwa ndefu zinavutia zaidi kuliko mwanzo zilikuwa kama misumari’

Alimmwagia sifa model kwenye video ya Lover Boy, anasema ametulia sana na amevaa vizuri

Kuhusu Sweet Mangi wa Nick wa Pili

Alisema alikuwa anajiuliza ni vipi Nick wa Pili alifahamu aina za nywele alizozitaja kwenye wimbo

Alidai G-Nako ameifanya video ya Sweety Mangi aipende zaidi

Kuhusu Kokoro wa Rich Mavoko f/ Diamond

Alimuelezea Mavoko kama msanii mwenye kipaji cha aina yake

Alisema alikuwa model kwenye video ya kwanza ya Mavoko ambaye anasema alikuwa anamuogopa hata kumshika Lulu

Alikiri kuwa video ya Kokoro haijambariki

Kuhusu Kajiandae wa Ommy Dimpoz na Alikiba

‘Ommy Dimpoz akikaa na Alikiba wana chemistry fulani hivi lazima wafanye kitu kizuri’

Aliwapongeza Ommy na Kiba kwa kuipa video mazingira ya Kiafrika zaidi

Kuhusu Muziki wa Darassa

Alisema Muziki ya Darassa umefanya vizuri bila hata kutumika nguvu nyingi

Alisema Muziki ni wimbo anaoupenda sana mama yake

Alimuelezea Darassa kama msanii mnyenyekevu asiyejisikia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents