Habari

Haya ni madhara ya Paracetamol kwa wanywaji sugu wa pombe

Unywaji wa pombe uliopitiliza huongeza hatari ya kupata homa ya ini (Athari mbaya za dawa kwa ini) pale unapotumia dawa aina ya Acetaminophen maarufu kama Paracetamol au Panadol.

Hii ni kwa sababu unywaji wa pombe hupunguza akiba ya “Glutathione” mwilini kemikali inayolinda chembe hai za ini. Ili acetaminophen itolewe mwilini haina budi kuvunjwa vunjwa na ini ilikupata kemikali ambayo itatolewa mwilini kupitia mkojo pale utakapokojoa.

Moja wapo ya zao la kuvunjwa vunjwa kwa acetaminophen ni N-acetylbenzoiminoquinone ambayo inatakiwa kuungana na Glutathione lasivyo itaungana na seli /chembe hai za ini na kuziharibu na kupelekea homa ya ini.

Hivyo basi kupungua kwa Glutathione mwilini kutokana na unywaji wa pombe kutaifanya kemikali hii hatari ipate nafasi ya kuungana na chembe hai za kwenye ini na kusababisha madhara.

Ikumbukwe kwamba unywaji wa pombe uliopitiliza peke yake ni hatari kwa afya ya ini lako, kwa hiyo unapochanganya na matumizi ya paracetamol hatari kwa ini huongezeka maradufu.

Peter Urio, Paul J Kirutu pamoja Abdillah Mnenge ambao pia ni wataalam waliobobea katika maswala ya dawa, vipodozi na utafiti wamesema sio lazima mtu ajioverdose kupata madhara yatokanayo na unywaji wa pombe na acetaminophen, hata katika dozi ya kawaida mtu anaweza kupata madhara makubwa ya kupata homa ya ini endapo atatumia pombe na paracetamol kwa wakati mmoja.

Nitoe wito kwa wanywaji wa pombe kupita kiasi kufikiria mara mbili mbili juu ya afya zao na maisha yao kwa ujumla.

Your Health, My Concern

BY FORD A. CHISANZA
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]
[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents