Burudani

Hawa ndio wasanii wanaompa changamoto Country Boy

Country Boy amewataja wasanii ambao wanaonekana kumpa changamoto kwenye muziki.

Raper huyo amewataja wasanii wanne kutoka Afrika Kusini ndio wanaompa changamoto huku kwa Bongo akimuona Bill Nas pekee.

“Ukimsikia Bill Nas unamsikia Emtee anauza, kuna Nasty C, KO, kuna Cassper Nyovest. Kwahiyo ukimweka na Bill Nas hiyo ndio challenge yangu, nafanya muziki ambao unatakiwa kuwa kiinternational,” amekiambia kipindi cha FNML cha EATV.

Kwa sasa rapper huyo yupo chini ya lebo ya LFLG inayoongozwa na Petit Man na Chakoma na tayari ameachia video ya wimbo wake wa kwanza ‘Hakuna Matata’ akiwa chini ya lebo hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents