Burudani

Hawa ndio wasanii 5 wa Bongo Flava anaowakubali Lulu Diva

Lulu Diva ambaye ni msanii mpya kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava amewataja wasanii watano wa muziki huo anaowakubali.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumatatu hii, muimbaji huyo amewataja wasanii hao kuwa ni pamaoja na Vanessa Mdee, Belle 9, Dogo Janja, Madee na Barnaba.

Diva ameongeza kuwa baada ya kuingia kwenye tasnia ya muziki hataacha kufanya kazi hiyo mpaka mwisho wa uhai wake huku. Kwa sasa msanii huyo ameachia wimbo wake wa pili ‘Usimwache’ ambao video yake imeongozwa na Nicrux kutoka Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents