Michezo

Hawa ndio wachezaji watakao kosa mechi ya Ujerumani na Uingereza

Timu ya taifa ya Ujerumani leo usiku March 22,2017, itawakosa wachezaje wake Mesut Ozil, Julian Draxler na Mario Gomez katika mchezo wa kirafiki dhidi ya England kutokana na majeruhi. Wakati huo pia Phil Jones amejiondoa katika kikosi cha Uingereza baada ya kuumia mazoezini jana.

Kocha wa kikosi cha Uingereza, Gareth Southgate amesema

“tumemrudisha Jones kataika klabu yake, tutajua zaidi baada ya vipimo katika saa 24 au 48 zijazo.”

Southgate hana mpango wa kumuita mchezaji mwingine kama mbadala ya beki huyo kwanza wataangalia hali yake baada ya mchezo wa kirafiki,katika kikosi chake ananjia mbadala ya mabeki wa kati ambao ni John Stones ,Michael Keane na Chris Smalling

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents