Habari

Tuzo za Kili kuoneshwa live kwenye screen kubwa uwanjani katika mikoa mitatu

Wataribu wa Tunzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Award, leo imekutana na wana habari kuwapa taarifa ya usiku wa utoaji tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award.

kavishe

Shughuli hiyo inatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City ulipo jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja usiku.yatakayokuwemo ndani ya Mlimani City ni pamoja na chakula cha jioni watakaokaa VIP na vitafunwa kwa watakaokaa kawaida. Utoaji tuzo unatazamiwa kuanza saa tatu kamili.

‘Zoezi la red carpet linatazamiwa kuanza saa moja kamili hadi saa mbili jioni ambapo chakula kitaanza mpaka saa tatu kamili shughuli itakapoanza”, alisema Bwana Kavishe.

“Tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia jumanne june 4, 2013 katika ukumbi wa Mlimani City Hall,Born to Shine Mwenge,Roby One Fashion Kinondoni na Sharks Limited Mtoni kwa Azizi Ali karibuni na Equator. “Naomba kusisitiza kwa Ticket za VIP zitauzwa ukumbi wa Mlimani City pekee na ziko chache sana kwa sasa hivi nawasihi wale watakaopenda kuhudhuria mnunue ticket zenu mapema.”

Kwa mwaka huu shughuli ya Mlimani City itaonyeshwa live na ITV na pia ili kuzisogeza tuzo kwa wananchi tumechagua mikoa michache ambapo zitonyeshwa kwenye screens kubwa katika maeneo tofauti katika mikoa mitatu.
Sehemu hizo ni Mwanza eneo la Mabatini, Temeke Uwanja wa Taifa na Kilimanjaro CCM Mkoa.”

Kavishe alisema zoezi la kupigia kura wasanii kuelekea tuzo hizo zinazokwenda na kaulimbiu ya Kikwetukwetu mwaka huu lilifungwa Mei 31, mwaka huu.

Kuhusu burudani katika usiku huo, Kavishe alisema kwamba wasanii wa sasa wataimba nyimbo za wasanii wa zamani na wasanii wa zamani wataimba nyimbo za wasanii wa sasa.

“Kutakuwa na kitu tofauti sana upande wa burudani, ambacho kitapendeza na kuvutia sana, kwa ujumla maandalizi yako vizuri na tunatarajia mambo mazuri siku hiyo,” alisema Kavishe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents