Habari

Hatimaye Reginald Mengi awakabidhi zawadi washindi wa ‘tweet’ zilizomgusa kwa mwezi May.

May 13 mwaka huu mwenyekiti wa makampuni ya IPP bwana Reginald Mengi alitangaza ulaji ambao ni kama wa bure, kwa kutangaza shindano la ‘tweet’, ambapo alisema kila mwezi atakuwa akitoa zawadi ya shilling million 1 kwa mtu atakaye andika tweet bora kushinda vita dhidi ya umasikini.

mengi washindi

Inawezekana wapo ambao walihisi kuwa huenda bwana Mengi alikuwa anatania, lakini amethibitisha ni kiasi gani hakua anatania baada ya jana (June 7) kuwakabidhi washindi watatu zawadi zao za pesa.

Bwana Mengi alimkabidhi mshindi wa kwanza Jilly Gaudence Kyomo zawadi yake ya shillingi millioni 1, aliyefuatiwa na mshindi wa pili ni Peter George aliyejishindia shillingi 500,000 na mshindi wa tatu Ludovick Angelino aliyejipatia shillingi 400,000.

Washindi hao walikabidhiwa zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya IPP jijini Dar es salaam, na baadae bwana Mengi alitweet kuwapongeza washindi.
tweet ya mengi

Kwa mujibu wa chanzo, bwana Mengi alisema shughuli ya kupata washindi hao ambao walichujwa kutoka katika tweet 481 zilizokuwa zilizopokelewa toka (Mei 13) siku alipozindua shindano hilo, ilisimamiwa na Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha Uongozi na Ujasiliamali (IMED), Donath Olomi na jopo lake.

Tweet iliyompa Jilly ushindi wa nafasi ya kwanza ilikuwa ‘Tuwe na utamaduni wa kupenda kile tukifanyacho, tukifanya kwa moyo, uadilif, heshima na kujali muda hata kama it’s self employed”, ambayo ilitimiza vigezo vya shindano ambavyo vilikuwa liwe wazo lililoeleweka na kuelezeka kirahisi, na lisiwe limeshasikika mara nyingi.

Haya kazi kwenu jamani shindano bado linaendelea kila mwezi kwa muda wa mwaka mzima so kuna miezi 11 mbele ya ulaji huo, washindi watakuwa wanakabidhiwa zawadi zao na kutangazwa.

Picha ni kutoka akaunti ya twitter ya Reginald Mengi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents