Habari

Hatimaye Juliana Kanyomozi wa Uganda ajiunga na Twitter!

Yawezekana ukashangaa kujua kuwa mwanamuziki mrembo kutoka Uganda Juliana Kanyomozi hakuwa na akaunti katika mtandao wa kijamii wa twitter, lakini huo ndio ukweli hakua amejiunga na twitter!.

JUliana-3

Katika ulimwengu wa sasa ni vigumu kwa watu wanaojihusisha na kazi za sanaa ambazo zinahitaji support ya watu wengi, kufanikiwa kuwafikia watu kwa haraka bila kuwa rafiki wa mtandao na kumiliki akaunti katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama facebook na twitter.

Mpaka mwaka huu 2013 hit maker wa ‘Usiende mbali’ Juliana Kanyomozi hakuwa na akaunti yoyote twitter kitu kilichokuwa kinafanya mashabiki wake kukosa mambo mengi na kuchelewa kupata habari juu ya kazi zake za muziki.

Wiki chache zilizopita Juliana akiwa anafanya promotion ya kazi yake mpya alifanyiwa mahojiano na Radio City ya Uganda, na mtangazaji wa kipindi hicho aitwaye McKenzie alipomuomba awaambie wasikilizaji official account yake ya twitter ili waweze kumfuata, Juliana hakusita kusema ukweli kuwa hajajiunga na twitter, na McKanzie akamuahidi kumfungulia akaunti.

Baada ya kupata msaada kutoka kwa mtangazaji huyo sasa Juliana Kanyomozi anapatikana kwa handle ya @JKanyomozi, na tweet yake ya kwanza ilikuwa (May 28) alipo tweet kuwataarifu fans wake kuwa hatimaye amejiunga na twitter.

Juliana 1st tweet

Mpaka leo Ijumaa (June 7) tayari Juliana ana followers 534 ikiwa ni siku ya kumi toka afungue akaunti hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents