Burudani

Hatimaye Diamond afanya collabo na Ne-Yo, asema itakuwa ‘hit song’

Kile kilichosubiriwa kwa hamu na mashabiki toka Diamond na Ne-Yo wakutane Afrika Kusini kwenye tuzo za MAMA 2015 hatimaye kimetimia, ni collabo ya Diamond Platnumz na mwimbaji huyo wa R&B kutoka Marekani.

diamond na Ne-Yo

Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram amemshukuru Ne-Yo baada ya kumaliza kurekodi wimbo huo. Katika picha aliyopost akiwa na Ne-Yo studio, pia anaonekana producer Sheddy Clever ambaye atakuwa amehusika na kazi hiyo.

“Thanks alot my Brother @neyo and the Whole Compound Crew had a great Session, and it was realy nice working with you…can’t wait for the World to hear this Hit Song!! @Diamondplatnumz ft @neyo ….. Cc @sheddyclever @Compoundu @thecorpshow @Jullianl #AfricaTotheWorld”

diamond post

dai-neyo

Dalili za kufanyika kwa collabo hiyo jijini Nairobi zilianza kuonekana siku moja iliyopita baada ya meneja wa Diamond, Salaam kuonekana kwenye picha iliyosambaa mtandaoni akiwa na Alikiba kwenye Coke Studio na kwa mbali akionekana Ne-Yo.

salaam na kiba

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents