Michezo

Harry Redknapp aitaja timu kubwa ya EPL inayoweza kukosa UEFA msimu ujao

Kocha mkongwe wa ligi kuu ya Uingereza, Harry Redknapp amefunguka kwa kuzitaja timu ambazo zinaweza zikakosa kuingia kwenye timu nne bora zitakazofanikiwa kucheza michuano ya UEFA msimu ujao.

Redknapp ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya taifa ya Jordan, ameitaja timu ya Liverpool kuwa ina uwezekano mkubwa kukosa michuano hiyo kutokana na kuweza kumaliza kwenye nafsi ya sita ya ligi hiyo huku akiacha karata moja kwa Man United na Man City.

“I look at that top six and I see them [Liverpool] finishing sixth. Why? Because I think Chelsea, Tottenham, Arsenal, Man City and Man United will finish above them – that makes them sixth! The other teams are stronger than them,” Redknapp told BT Sport.

“It’s between Liverpool, Man United and Man City who makes that top four. Two of them will miss out. The three London teams will finish first, second and third,” ameongeza.

Kwa sasa Liverpool inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 45, Man City inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 43 na Man United inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 41 huku ligi hiyo ya Uingereza ikiongozwa na Chelsea yenye pointi 55 ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 47.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents