Burudani

Harmonize awajibu wanaoiponda script ya video ya Niambie

Ni wiki moja sasa tangu First Born wa WCB,Harmonize apandishe Youtube video yake mpya ya Niambie ambayo imeonekana kupondwa na baadhi ya watu kuwa haijaendana na maudhui ya audio.

Watu wengi wanadai kuwa audio inajenga picha ya umaskini,lakini kwenye video Harmonize anaonekana kwenye maisha ya kishua sana,jambo ambalo limewakera baadhi ya mashabiki.

Kwenye interview na Prince Ramalove kupitia Kings Fm, mkali huyo amefafanua maana ya script ile ya video.

“Sina mtonyo lakini naishi kwake,sasa nikiishi kwake na yeye ana hela,ntafanyaje?”a mefafanua Harmonize. Kwa maelezo hayo mafupi,ni kwamba nyumba na magari yanayoonekana kwenye vdeo ni mali za Wolper kwa mujibu wa script.

Pia Harmonize alipoulizwa kuhusu kumuoa Wolper, alijibu kifupi tu ‘Suprise.’

By Prince Ramalove
Kings Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents