Burudani

Hanscana aenda Afrika Kusini kutafuta connection za kimataifa na kuongeza ujuzi kwa Justin Campos (picha)

Muongozaji na mtayarishaji wa video Hanscana yuko nchini Afrika Kusini, alikoenda kwaajili ya kuongeza ujuzi pamoja na kutafuta connection za kuwezesha kazi zake zifike kwenye vituo vya runinga vya kimataifa.

Hanscana na campos-5
Hanscana akiwa an Justin Campos na mkewe Candice

Wiki hii Hanscana amekuwa akipost picha mbalimbali Instagram akiwa na director Justin Campos na mke wake Candice Campos ambaye pia ni producer wa video wa kampuni ya Gorilla Films.

Hanscana amepiga story na Bongo 5 na ametueleza kilichompeleka Afrika Kusini:

“Unajuwa sasa hivi game imechange kwa kiasi kikubwa sana na unaweza kuliona hilo kama director/msanii una Malengo MAKUBWA na unaona mbali. Na kila masanii kwa sasa anataka kazi yake ifike mbali na kwa gharama yeyote ile ( kwa kila hali ) ndo maana unaona wanajaribu kufanya kazi na directors wa nje ili waweze kufikishiwa kazi zao katika level zinazostahili” amesema Hanscana.

Hanscana na campos-3

Ameendelea,

“Nikiwa kama director ambaye hata mimi pia ninahitaji kazi zangu zifike level zinazostahili kufika, basi ni jukumu langu kuhakikisha natafuta njia za kufikisha kazi zangu huko ili niweze kuendana na soko la muda huu linavyotaka na sio kukaa nyumbani na kuanza kulalamika ‘oh wasanii sio wazalendo wanapeleka hela kwa directors wa nje’ “ alifafanua Hanscana.

Hanscana na Campos-1

Ukaribu wa Hanscana na Campos ulianza muda mrefu, ambapo pia Hanscana na Khalfani waliwahi kuwa wenyeji wa Campos alipokuja Zanzibar kushoot video ya wasanii wa Ghana.

hans sa

Kingine anachokifanya Afrika Kusini ni kushoot video na wasanii watatu ambao hawajapenda kutajwa kwa sasa.

hanscannn

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents