Michezo

Hamisi wa Ndanda FC achaguliwa mchezaji bora wa mwezi Novemba

Mchezaji Riphat Hamisi wa timu ya Ndanda FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Novemba kwa msimu wa 2016/2017.

Riphat ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Shaban Idd wa Azam FC na Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar.

riphat
Mchechaji Riphat Hamisi ni wakulia akikimbilia mpira

Katika mechi mbili ambazo timu ya Ndanda FC ilicheza kwa mwezi huo, Riphat aliisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo yote na kukusanya jumla ya pointi 6 zilizoifanya kushika nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi hiyo ambayo iko mapumzikoni kupisha dirisha dogo la usajili.

Pia aliifungia timu yake mabao mawili katika michezo miwili ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo.

Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili zilizochezwa. Kwa kushinda tuzo hiyo, Riphat atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents