Habari

Halmashauri ya jiji la Dar es salaaam kuruka na,City FM,hewani rasmi wiki hii


Kituo cha radio kinachomilikiwa na halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, City FM 91.3, kinatarajiwa kuwasha rasmi wiki hii.
Mmoja wa wasimamizi wa kituo hicho ambaye hakutaka kutajwa jina lake ameiambia Bongo5 kuwa maandalizi yote muhimu ikiwa pamoja na studio na vitambulisho vya sauti vya radio (Station Identification/jingles) yameshakamilika.
Amesema radio hiyo inatarajiwa kuwa ya kibiashara kama zilivyo radio zingine hapa nchini na kwamba City FM itakuwa radio huru isiyofungamana na upande wowote.
Studio za City FM zipo kwenye ofisi za halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Kama kikiendeshwa vizuri, kituo hicho cha radio kinaweza kuwa chanzo kingine kikubwa cha mapato ya jiji la la Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents