Burudani

Halima Mdee: Kajala na Lulu wanahitaji second chance


Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Halima Mdee, jana kupitia Twitter alisema kuwa Lulu na Kajala waliopo gerezani Segerea wanahitaji nafasi ya pili na kwamba kama wakitoka watakuwa wamebadilika kwa kiasi kikubwa.

“Nilikwenda gereza la Segerea, pamoja na mambo mengine nilifanikiwa kuongea na Lulu na Kajala. Natamani wangepata 2nd chance,” alitweet.

“Mazungumzo yangu nao yamenidhihirishia kwamba wakipewa nafasi ya pili,watakuwa sio watu ambao tumewazoea. Wanataka anza upya!”

Naye mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhaji aliongezea kwa kusema, “Kila mtu anastahili second chance…hakuna binadamu aliyekamilika! God bless!!”

Lulu anakabiliwa na kosa la mauaji ya Stephen Kanumba huku Kajala na mumewe wakikabiliwa na makosa kadhaa likiwemo la kula njama kwa kuhamisha umiliki wa nyumba, kutakatisha fedha haramu miongoni mwa makosa mengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents