Habari

Hakuna tatizo la njaa nchini – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ametoa wito kwa Watanzania kupuuza baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotoa taarifa kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la njaa huku akisema kuwa anayejua njaa ni Rais.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi mkoani Simiyu Rais Magufuli amesema kuwa taarifa hizo ni uzushi huku akisema kuwa kama yeye Rais wa Tanzania yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za njaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

“Wapo wafanyabiashara wengine wachache waliokuwa wamezoea panapotokea matatizo kidogo tu ya ukame wanatumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na magazeti wanayoyaamini wao sio magazeti yote, pamoja na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa, anayejua njaa ni Rais na sio gazeti fulani mimi ndiyo niliyepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania,” alisema.

Hivi karibuni kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita aliitaka serikali kutangaza balaa la njaa.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents