Habari

‘Hakuna mgonjwa wa Ebola Tanzania’ asema Waziri wa Afya

Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa kuna watu wawili, mmoja raia wa nje na mwingine Mtanzania kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, serikali imethibitisha kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini. Imesema wagonjwa waliohisiwa awali, walikuwa na magonjwa tofauti.

Dr-Seif-Rashid
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Rashid

Akizungumza leo asubuhi na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashid amesema wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizi kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania.

“Kuna wagonjwa ambao tumewalaza lakini kwa mujibu wa dalili walizokuwa nazo na vipimo vilivyofanyika hawana hali ya kuwa na ugonjwa wa Ebola,” amesema Dr. Seif. “Kwenye hali kama hii ambapo tunakuwa na hali kubwa ya kuweza kuhakikisha mtu ambaye anaweza akawa na dalili za ugonjwa, lazima tuweze kumuona na kumpima ili tujihakikishie kuwa hana tatizo. Lakini kiukweli sasa hatuna mgonjwa mwenye tatizo la ugonjwa wa Ebola. Tulikuwa tuna wagonjwa wawili mmoja ni binti ambaye ametokea Benin na alivyofika kwenye hospitalI ya mtu binafsi na dalili za kuwa na homa kali na viungo na maumivu kama hayo lakini baada ya kumchuKUa mgonjwa na kufanya vipimo zaidi ikajulikana ni mgonjwa mwenye matatizo ya malaria tu na kwamba hana tatizo la ugonjwa wa Ebola,” amongeza.

“Huyo mgonjwa tumemuondoa hana tatizo hilo. Na mgonjwa mwingine ni mgonjwa ambaye ana tatizo lingine kabisa ambalo linakuwa linapelekea kutoka damu, kwahiyo nafiriki katika kitendo hicho cha kuonekana anatoka damu kikahusishwa na hilo. Lakini kwa ujumla wagonjwa wote wawili hawamo katika tasfiri ya ujumla za dalili zile za ugonjwa na namna ambavyo tunaweza kuweka katika kundi la magonjwa haya ya Ebola huyu ni Mtanzania.”

Pia jana Dr Seif alitweet:

Msikilize zaidi hapa:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents