Burudani

Hakuna beef: Iggy Azalea ampongeza Nicki Minaj backstage MTV-VMA (video)

Baada ya kuwepo na tetesi za beef kati ya rapper wa kike mzaliwa wa Australia Iggy Azalea na Nicki Minaj, marapper hao Jumapili iliyopita (Agosti 24) walikutana backstage kwenye tuzo za MTV VMA na kuziuwa kabisa tetesi hizo.

http://youtu.be/70jEETebrEA

Baada ya Nicki kuperform single yake mpya ‘Anaconda’ akiwa anajiandaa kuhojiwa na MTV backstage ndipo Iggy alipita na kumpongeza kwa kumwambia “You did great,” , na Nicki akamjibu “Thank you honey,” huku akiwa na tabasamu kubwa usoni.

Hisia za kuwepo kwa beef kati ya Nicki na Iggy zilikua zaidi baada ya kauli aliyoitoa Nicki wakati wa tuzo za BET, ambayo baadae alikuja na kujitetea kuwa vyombo vya habari vilimuwekea maneno mdomoni.

Hata hivyo Nicki Minaj pia aliwahi kumpongeza Iggy Azalea hadharani kwa mafanikio ya single yake ya ‘Fancy’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents