Burudani

‘Habari za Diamond kutudhalilisha ni za uongo’ asema msanii wa Mombasa aliyeripotiwa kufukuzwa VIP Lounge (Audio)

Msanii maarufu wa mjini Mombasa, Kenya, Susumila amekanusha taarifa zilizotapaa mjini humo kuwa yeye na Nyota Ndogo walidhalilishwa na Diamond pamoja na mwandaaji wa show yake iliyofanyika huko weekend iliyopita.

wpid-diamond-alipanda-na-gwanda-za-jeshi.jpg

Mtandao wa Standard Media wa Kenya, uliandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na Nyota Ndogo waondelewe.

Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake na kwambatukio hilo liliwafanya wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani waandaji wa show hiyo ambapo VJ Delph alikataa kucheza muziki.

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto, Willy M Tuva wa Radio Citizen leo, Susumila amedai kuwa hizo ni habari za uzushi.

Susumila
Susumila

“Hizo story ni za uongo,” amesema msanii huyo. “Sidhani kama Diamond anaweza kufanya hivyo au ana haki ya kufanya hivyo. Kama nimekuwa mistreated labda niwe mistreated na yule mtu amenipatia show, sio Diamond sababu naye ameitwa kwenye show kama mimi,” ameongeza.

“Unajua Mombasa wanapenda vitu vya uongo, hakuna mtu ana complain kuhusu show ilikuwa mbovu ama nini, watu wanatafuta vijisababu vidogo vidogo wanasema sijui nimenyimwa maji. Mimi nilipanda steji nilikuwa na chupa yangu ipo kwa DJ, nikaperformm dancers wangu walipokuwa wameingia wanafanya set yao nikachukua maji nikanywa pale pale kwa DJ kulikuwa na chupa kama kumi za maji hazijafunguliwa. Sijui story ilianzia wapi lakini kufikia kwenye saa tatu, saa nne ilikuwa kwenye blog karibu zote za huku (Mombasa).”

Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents