Habari

Habari ya Moto hoteli ya Naura Springs Arusha yaigeuza July 18 remix ya April 1!!

Katika ulimwengu huu huru wa mitandao ya kijamii usiamini kila kitu unachokiona kimeandikwa. Hata kama kikiwa na picha inayoyashawishi macho yako kuamini, chunguza kwanza kwa muda wako kabla ya kuthibitisha uhalali wa kile ukionacho.

1366032517_DSC03516
Muonekano wa hoteli ya Naura Springs ya Arusha

Na kwa wenye fani ya uandishi wa habari, kama ni tukio linalohusu majanga, basi hatu ya kwanza ni kufanya ‘verification’ kupitia mamlaka husika. Usiharakishe kuandika habari ili kuwania kuwa wa kwanza kuripoti kwakuwa mambo yanaweza kugeuka.

Jana kulisambaa habari ya kwamba hoteli ya kifahari ya Naura Springs ya jijini Arusha inateketea kwa moto. Habari hiyo iliyokuwa maarufu Facebook, ilikuwa na picha mbalimbali zinazoonesha jengo la ghorofa likiwaka moto tena kwenye floor ya juu kabisa. Kama ingekuwa imeandikwa na watumiaji wa Facebook wasio na majina nchini, wengi wasingeichukulia kwa uzito wowote, lakini kwakuwa waliopost picha hiyo ni watu wenye nafasi kubwa za kuhabarisha wananchi, wengi waliamini.

Vyombo vya habari vikubwa navyo pia viliingizwa mkenge na picha hiyo japo vile vyenye waandishi wadadisi, vilisita kwanza kuandika na kuzipigia simu mamlaka husika kuulizia kama kweli hoteli hiyo inateketea kwa moto.

Bahati mbaya habari hiyo haikuwa kweli, na kama unavyoweza kuhisi, ni kweli imesababisha usumbufu mkubwa kwa uongozi wa hoteli hiyo na huenda biashara haikuwa nzuri jana. Kufuatia usumbufu huo, uongozi wa hoteli hiyo umedhamiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu/watu waliosambaza habari hizo.

“Utawala na wafanyakazi wa hoteli ya Naura Springs imesikitishwa kwa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kuwa hoteli yetu inawaka moto na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watu wa mkoa wetu, ndugu na jamaa wa wafanyakazi wa hotel ,viongozi mbalimbali, vyombo vya usalama, idara ya zima moto, waandishi wa habari wa vyombo mbali mbalii vya habari na pia kusababisha wasiwasi na kutowesha utulivu na amani wa mji wetu,” alisema meneja wa hoteli hiyo Beatrice Dimitris Dallaris kwenye maelezo kwa vyombo vya habari.

“Tumesikitishwa sana na tumeomba uongozi wa mkoa wetu walishughulikie swala hili kikamilifu kwani hili sio la kuchukulia mzaha na Tungeomba hatua kali zichukuliwe kwa haraka sana kwa alie toa taarifa hiyo ya uongo. Tunawashukuru watu wote Waliofuatilia swala hili napia tunatoa tamko kuwa habari hizi za kuwa hoteli yetu inaungua ni za uongo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents