Burudani

H.Baba: Ndoa yangu na Florah inapigwa vita sana

H.Baba anadai kuwa maisha ya ndoa na mke wake Florah Mvungi hayakuwa rahisi siku za mwanzo kwakuwa walikutana na vikwazo vingi.

H.Baba akiwa na mke wake Frora Mvungi

H.Baba amesema pamoja na kupigwa majungu na watu, familia yake imeendelea kuwa imara.

“Wasanii wengi sana ambao walikuwa karibu na wife walitaka kuharibuharibu na baadhi ya wasanii waliweza kuongea maneno mengi, wengine tunakupa mwaka, wengine mwezi, lakini wao sio Mungu wao ni mashetani tu,” ameiambia Bongo5.

“Ukiweza kufuatilia maisha ya mwenzio, wewe ni shetani. Kwa sababu wewe huna maamuzi na huna mamlaka. Kwahiyo walipiga sana majungu na fitna bado zinaendelea. Wengine wanadiriki kuongea na watu nyimbo za H.Baba sizipigwe. Wengine walifanya vyovyote ili nisifikie maisha fulani. Yaani kuna changamoto kibao nakumbananazo kwa sababu walikuwa wanataka kutufelisha. Lakini kwa sababu wao sio Mungu na Mungu ndio anayejua mwisho wa maisha yetu lakini sio wao. Ninachoweza kuwaambia watahesabu siku sana kwa sababu wao sio Mungu.”

H.Baba aliandelea:

“Hii sanaa sio ugawe mwili wako ndo ufanye sanaa na ujione wewe ndo msanii mkubwa sana. Sanaa ni heshima na wewe ni kioo cha jamii. Unapotumika sana mwisho wa siku hutakiwi. Kuna miaka mitatu mbele ya kufagiliwa na watu lakini baadaye wanaokota takataka wanaweka pembeni basi yaani huo ndo mwisho wako. Kwahiyo mke wangu hayupo kama wao, anajiheshimu na anatambua nini anafanya ndio maana hata muziki akifanya akimaliza anapumzika sio kutumikatumika kama wao wanavyotumika. Kwahiyo wakiongea wakisema nini mke wangu namtengezea ninavyotaka kwa sababu tayari nimeshakabidhiwa mzigo na nina umiliki. Kwahiyo muziki wetu, filamu zetu, hapa ni kwenda mbele tu hatuwapi tena watu nafasi kwenye maisha yetu ya kazi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents