Burudani

H.Baba: Mwanangu Tanzanite ana meneja wake na ‘soon’ ataanza kufanya matangazo

H.Baba hataki mchezo. Muimbaji huyo wa mtindo alioupa jina ‘Bongo Bolingo Flava’, amesema mwanae wa kike, Tanzanite ana meneja wake anayejitegemea.

H.Baba na mwanae Tanzanite
H.Baba na mwanae Tanzanite

Akizungumza jana kwenye kipindi cha The Mboni Show cha TBC 1, H.Baba, alisema yeye na mke wake watakuwa hawahusiki kwenye biashara zitakazojitokeza kwa mtoto wao huyo.

“Mke wangu ana meneja wake na ana menejimenti yake kabisa ya muziki,” alisema. “Mimi niko chini ya Dr Fadhili wa Fadhaget Clinic ndio wanasimamia shughuli zangu zote za muziki na mambo yote. Mtoto Tanzanite ana meneja wake pia kwa sababu kuna matangazo ambayo anatakiwa kufanya, sasa tumempa meneja wake. Kwahiyo kila mtu ana menejimenti yake katika familia hii.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents