Burudani

H.Baba kumfunza binti yake kutumia keyboard, asema akianza kuongea atampeleka studio

Muimbaji Hamis Baba maarufu kama H.Baba amemnunulia vifaa vya muziki binti yake, Tanzanite na kuanza kumfunza kuvitumia. Pia amesema mwanae huyo akianza tu kuongea atampeleka studio.

o

H.Baba amesema mwanae huyo ana kila dalili za kuja kuwa mwanamuziki kama wazazi wake.

“Mwanangu mimi ana dalili zote za kuja kuwa mwanamuziki kwa sababu kila kitu anakionyesha,” H.Baba ameiambia Bongo5. “Nimemnunulia keyboard lakini nimemwachia ndani kaanza kubinya mwenyewe anajua nikibonyeza hapa inalia hii na hii. Mimi nakuwa namwonyesha piga hapa piga hapa. Yaani namuomba mwenyezi Mungu tu akiweza kuchanganya maneno tu basi anaingia kwenye muziki moja kwa moja.”

10684001_741698622568253_1648999241_n

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents