Burudani

H.Baba atoa ushauri kwa wasanii wanaotaka kugombea ubunge na nafasi zingine

H.Baba amewatahadharisha wasanii wa muziki nchini waliotangaza au waliopanga kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao kuwa wakikosa nyadhifa hizo watapotea kabisa kwenye muziki.

Rais wa shirikisho la wasanii Ado Novemba akimkabidhi tuzo ya msanii bora wa kutumbuiza H.Baba

H.Baba amewataka wasanii kuacha kukurupuka kwani katika siasa mgombea anatakiwa awe amejianda kisaikojia ili kukabiliana na matokeo yake.

“Wasanii wenzangu mimi nawashauri ingawa kila mtu na mtazamo wake, lakini siasa ni kipaji sio kuparamia. Sasa usimuone mwenzio amefanikiwa na wewe pia utafanikiwa, hapana jiangalie kwanza una kipaji cha kuzungumza? Una kipaji cha kukubalika? Je? Unaweza kweli ukafaulu hilo jambo unalotaka kulitimiza au lah? Sio kukurupuka tu,” amesema H.Baba.

“Ukishindwa ni aibu na kimuziki utashuka. Kama unajipa asilimia mia za ushindi inabidi ndo ukomae ili ushinde maana mambo ya siasa nayo yana kipaji. Mimi huko sipo, mimi kazi yangu ni muziki tu kuburudisha watu tu. Kwenye siasa mimi huko sipo, siasa nawaachia wanaoweza. Kuna wasanii nimesikia wanagombea, mimi binafsi nitawa support kwa sababu wana uwezo na pia wana kipaji, kwa sababu sio kila mtu ana kipaji kimoja, kuna watu wana vipaji zaidi ya vitatu kwahiyo wanaweza kuvitumia pia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents