Michezo

Guardiola ameonya watu wasimlinganishe Saul na Messi

Kocha wa timu ya Bayern Munich, Pep Guardiola ameonya watu walioanza kumlinganisha Saul Niguez na Messi.

saulniguez-cropped_fm5j6q35n6tq1xv19mtq4349l

Saul jana usiku aliifungia Atletico Madrid goli pekee ambalo liliifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bayern waliokuwa ugenini kwenye uwanja wa Vicente Calderon.

Baada ya mechi hiyo Guardiola alisema, “Binafsi simjui vizuri, lakini naheshimu ubora alio nao Saul. Lakini itakuwa vema kwake kutomlinganisha na Messi. Alichofanya Saul kinaweza kutokea.”

Guardiola alisema timu yake ilihitaji walau goli hata moja lakini bado wananafasi nyingine ya kutetea nafasi yao ya kucheza fainali ya Uefa kwenye mchezo wa marudiano utakao fanyika wiki ijayo kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents