MichezoMuziki

Griezmann asema hana mpango wa kwenda Manchester United

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann, ameitakatisha tamaa Manchester United inayotajwa kuwa katika harakati za kumsajili mwishoni mwa msimu huu, kwa kusema hana mpango wa kuondoka mjini Madrid kwa sasa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amekua chaguo la kwanza la Jose Mourinho kuelekea usajili wa majira ya kiangazi, lakini kauli yake ya kusema bado ni mwenye furaha huko Vicente Calderon inafuta harakati hizo.

“Mustakabali wangu? Binafsi ninategemea kuuonyesha uwanjani na sio sehemu nyingine katika maisha yangu, sina mpango wa kuondoka Atletico Madrid na ninafurahia maisha ya klabu hii,” Griezmann aliiambia Telefoot.

“Ninasisitiza tena, ninafurahia maisha ya mji wa Madrid. Hakuna kitakacho badilisha msimamo wangu.”

Juma lililopita meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hatompangia wala kuweka msimamo kwa mshambuliaji huyo kubaki au kuondoka klabuni hapo.

Alisema Atletico Madrid ilishawahi kuwa na washambuliaji waliosiofika duniani kama Sergio Aguero, Falcao na Diego Costa lakini waliondoa Vicente Calderon.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents