Burudani

Gosby auelezea mstari wenye utata kwenye ‘Just Pretend’ anaodai anayemuiga anasifiwa kuliko yeye

Rappers Gosby na Wakazi wameshirikishwa na Mic Lon kwenye wimbo wake ‘Just Pretend’ uliotoka jana. Kwenye verse ya Gosby kuna mstari wenye utata usemao ‘Leo anasifiwa mtu ambaye ananiiga’. Tumetaka kufahamu ni rapper gani anayemuiga na haya ndio majibu ya Gosby.

CD101

“Watu wanatumia zile wanaziita subliminal kwahiyo mtu ambaye inamgusa huwa anajua kabisa. Kwahiyo mtu atakuwa anajijua au watu watakuwa wanajijua, sio mtu mmoja tu kibao,” amesema. “Mtu mwingine anaiga flow lakini anaibadilisha kidogo tu, anaitwist. Kuna watu wengi huwa wanakubali na wanasema kabisa kwamba ‘mtu fulani mimi ndio ameniinspire, hii flow nzima nimeipata kwa mtu fulani. Lakini Kibongobongo inakuwa ngumu, unamsikia mtu anafanya interview halafu anarap kama wewe au anajitahidi kurap kama wewe lakini unamsikia ‘aah bwana mimi ameniinspire 50 Cent, ama Snoop Dogg’ I am like yo man why? Wakati unaflow kama mimi!”

Gosby amesema hatishiki anaposikia mtu akifanya style kama yake kwakuwa hiyo humfurahisha japo kinachomuumiza ni watu kutosema ukweli.

Usikilize wimbo huo hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents