Burudani

Godzilla: Huwezi kulinganisha video za Afrika Mashariki na za Nigeria na Afrika Kusini, kususia tuzo za MAMA ni ‘utaahira’

Rapper Godzilla amesema ni ngumu kulinganisha video za wasanii wa Afrika Mashariki na zile za Nigeria na Afrika Kusini na ndio maana wasanii wa nchi hizo wamepata nominations nyingi kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards, MAMA na hivyo kama kuna wasanii wamepanga kuzisusia watakuwa hawana akili nzuri.

Godzilla akichana.

Akijibu swali kama ni sahihi kwa wasanii wa Afrika Mashariki kutozipa ushirikiano tuzo hizo, Godzilla amesema: Ukiangalia video za East Afrika kiusemaukweli hatuwezi kuziweka na video zile zinazofanywa na akina Davido. Let’s be honest, machizi wana bajeti kubwa wanafanya video za hela nyingi kali na ndio zinaenda. Ingekuwa music awards ya audio tungesusia sababu tungesema ‘na sisi tuna audio kali’ lakini zinaenda za kwao sababu wanafanya video kali. It’s MTV Music Awards, sio audio. Hao jamaa wana video kali let them go.”

Godzilla amesema kususia tuzo sio uamuzi mzuri bali wasanii wa Afrika Mashariki wanatakiwa kujipanga kwa kuboresha video zao. “Kususia ni utaahira, ukosefu wa nidhamu na kushindwa, hizo ni kauli za kushindwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents