Burudani

Godzilla apanga kupunguza kufanya collabo mwakani

Rapper wa Salasala, Godzilla amedai kuwa mwaka ujao atafanya muziki wake kibiashara zaidi ikiwa ni pamoja na kupunguza kufanya collabo zisizo na maslahi.

wpid-godzilla-karibu-yako.jpg.jpeg

Godzilla ni miongoni mwa wasanii wanaoshirikisha zaidi nchini.

“Mwaka ujao utakuwa mwaka tofauti sana kuanzia kwenye utoaji wa muziki wangu, mwakani ni video na audio,” ameiambia Bongo5. “Kwahiyo kuanzia mwaka ujao haitatoka nyimbo isiyokuwa na video, itakuwa sio story tena ni kazi tu, muziki, video, audio na haitakuwa na range ya muda mrefu labda ni miezi mitatu au miwili.”

“Collabo tunaangalia zenye faida, vitu fulani vitabadilika itakuwa moja kwa moja ni biashara. Collabo zitapungua, kama nafanya kazi na wewe najua tuta-push wote yaani lazima kolabo iwe na kitu. Isiwe hivi hivi nimefanya ilimradi nimepita. Kwahiyo collabo nitafanya chache kadri ninavyoweza.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents