Burudani

Godzilla adai Hip Hop ya Tanzania haina ushindani tena, amsifia Nay wa Mitego

Godzilla anaamini kuwa muziki wa Hip Hop nchini hauna tena ushindani kwakuwa wasanii wengi wamekuwa marafiki sana na hivyo kushindwa kupeana challenge.

DJ Choka, Salama Jabir na Godzilla

Rapper huyo wa Salasala ameiambia Bongo5 kuwa hip hop ya sasa imekuwa ya biashara zaidi na sio kama sanaa.

“Hatukatazwi kuwa pamoja. Unajua Hip Hop inahitaji kupena challenge sana ili kila mtu uwezo wake uonekane sio kuandika maishairi tu ya kuelimisha. Ili Hip Hop ichangamke lazima iwe normal. Mfano kama bongo fleva wanavyopeana challenge, unajua napenda kama anavyofanya Nay wa Mitego, analeta challenge vile anavyosema fulani hivi fulani vile, ndo iwe vile. Lakini iwe kiamani sio lugha mbaya,” ameongeza Zizi.

Zizi pia amezungumzia wimbo aliofanya na Diamond, ‘Mtoto wa Mama’.

“Unajua siku ile tulikuwa studio na Marco chali tunapeana freestyle,” amesema. “Kumbe tunaweza kufanya kitu basi beat ilikuwepo pale kila mtu sasa akawa anaandika mistari yake kwa kujificha kwa kuogopa kufunikana si unajua tena ila Diamond alinisurprise sana alivyochana na ameitendea haki ile ngoma.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents