Burudani

Godzilla adai bila kuwekeza kwenye video nzuri, muziki wa Tanzania hauwezi kwenda popote

Rapper wa Thank You, Godzilla amesema kama wasanii wengi wasipokuwa ‘risk takers’ mfano wa AY, ni vigumu muziki wa Tanzania kufanya vizuri kimataifa.

Godzilla

Amesema ili wimbo wowote hata kama ni mzuri uweze kwenda kimataifa, ni lazima uwe na video kali. Hata hivyo amesema video kali ina gharama kubwa.

Akiongea na Bomba FM kwenye kipindi cha Kali za Bomba, Godzilla amesema upande wa audio hatuna tatizo na huenda tukawa sawa na Nigeria ambao wametuzidi kwa kutoa video kali.

“We need quality videos, na bajeti ya quality video ni kuanzia milioni 10 huko, milioni 15,” alisema.

“Kama unataka kwenda mbali zaidi inabidi uanze kuwekeza kwenye muziki wako. Watu hawajawa willing kutoa milioni 15, nikapate video moja kwenda Afrika nzima, watu bado wanaogopa risk wakati entrepreneur mzuri ni yule anayechukua risk, yaani huogopi.” Huwezi kuwa na quality ya video ya milioni 1 ukataka kwenda kupiga milioni 800, wekeza hela nyingi upate hela nyingi.”

Aliongeza pia kuwa waongozaji wengi wa video za muziki wa hapa Tanzania hutumia vifaa duni na hivyo sio rahisi kufanya video zenye viwango vya kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents