Burudani

Ginuwine yupo mbioni kutangaza kufilisika

Mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri kwenye muziki wa R&B mwishoni mwaka miaka ya 1990s mpaka mwanzoni mwa 2000, Genuwine anakaribia kufilisika, kwa mujibu wa mwanasheria wake, aliyetoa kauli juu ya kesi ya madai inayomkabili Ginuwine iliyofunguliwa na Robert Reives, aliyekuwa executive producer album yake iliyotamba, The Bachelor.

10384524_1564289543786981_8355500609469202466_n

Inaonesha kuwa Ginuwine, ambaye jina lake halisi ni Elgin Baylor Lumpkin atatangaza kufilisika kwake muda wowote kuanzia sasa.

“Mr. Lumpkin is very close to declaring bankruptcy. He owes my firm a ton of money and a bunch of other people a ton of money. He owes Uncle Sam 300-odd thousand dollars in back income taxes,” mwanasheria Bruce Beckner, ameeleza. Beckner pia amesema Ginuwine anakabiliwa na matatizo ya kifedha baada ya kutalikiana na mke wake Solé.

Kupitia madai ya kesi hiyo, mtayarishaji Reives anataka kulipwa kiasi cha dola milioni 1.25 kama deni la mrahaba wa albam tano za msanii huyo alizotayarisha wakati akiwa chini ya lebel ya Sony. Ginuwine na mtayarishaji huyo wamekuwa kwenye malumbano ya madai ambayo yanaonesha kumkwaza Ginuwine. Kesi itaendelea tena Jumatatu November 17 katika mahakama ya Manhattan Federal Court.

Akiba ya msanii Ginuwine inatajwa kuwa imeshuka mpaka kufikia kiasi cha dola milioni 11.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents