Habari

Gharama za kupanga nyumba Dar ni aghali kuliko miji mingine ya Afrika Mashariki

Kupanga nyumba nzima ya kuishi katika maeneo ya watu wazito jijini Dar es Salaam kuna gharimu fedha nyingi zaidi kuliko miji mingine ya Afrika Mashariki.

32959eac30c9228be9095955cbe062ac

Kupanga nyumba/chumba yenye ukubwa wa square foot 900 kwenye maeneo kama Masaki, Mbezi ama Osyterbay jijini Dar es Salaam inagharimu hadi dola 2,711 ambazo ni kama shilingi milioni 4.3 kwa mwezi ukilinganisha na Nairobi, Kigali na Kampala.

Kwa mujibu wa mtandao wa expatistan.com unaoangalia gharama za kuishi katika miji mbalimbali duniani, nyumba yenye ukubwa hiyo inagharimu dola 1,247 jijini Nairobi, dola 1,182 jijini Kampala na dola 933 jijini Kigali.

Mtaalam elekezi (consultant) wa masuala ya nyumba wa kampuni ya GimcoAfrica, Sultan Mndeme amesema sababu ya nyumba za Dar katika maeneo hayo kuwa aghali, ni kutokana na mji huo kuwa na maeneo machache yaliyopangwa na yanayotoa huduma za uhakika za maji, barabara nzuri na yale yasiyo na msongamano.

“Wateja siku zote hushindania maeneo machache na hiyo huongeza gharama za kodi katika maeneo hayo,” Mndeme ameiambia safu ya Business Week ya gazeti la The Citizen.

Mndeme amesema wamiliki wengi wa majengo jijini Dar es Salaam huwalenga zaidi watu wenye kipato cha juu na kuwasahau wale wanaopata kipato cha kawaida na wahitimu wa vyuo vikuu. “Nalishauri shirika la nyumba Tanzania na masharika ya mifuko ya uzeeni kubuni miradi ya nyumba za bei za chini kwa watu wenye kipato cha kawaida.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents