BurudaniVideos

Genevieve (Miss TZ 2010) azungumzia kuingia kwenye muziki, baba yake kumiliki bendi iliyokuwa na nguli Nguza, Zahir Zorro na King Kiki (Video)

Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, ameingia rasmi kwenye muziki na wimbo wake wa kwanza unaitwa Nana.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo amedai kuwa muziki ni kitu alichopenda kuja kukifanya tangu apate akili ya kutambua nini anapenda maishani mwake. Anasema mapenzi ya muziki ni kitu kilichopo kwenye familia yao kwakuwa hata baba yake mwaka 1986 alikuwa na bendi iitwayo Sambulumaa.

“Katika hiyo bendi yeye ndiye alikuwa owner wa bendi lakini ilikuwa managed na Nguza, ambapo ndani ya hiyo bendi alikuwepo msanii mkongwe kabisa King Kiki, alikuwepo pia na Zahir Ally Zorro,” amesema.

“Kwahiyo muziki ni kitu ambacho yaani nimekua katika surrounding hiyo,” ameongeza.

Pia Gene anadai kuwa kaka yake, mtoto wa kwanza kuzaliwa kwenye familia yao, alikuwa na kundi lake liitwalo DNT na mwaka 2000 walirekodi wimbo uitwao ‘Hanitaki Tena.’

“Danny (kaka yake) was a singer, Trigger was a rapper. Lakini katika hii nyimbo walifanya rap session ambayo ilifanywa na Jose Mtambo, it’s a very nice song.”

“On a personal level, muziki ni kitu ambacho kinanifanya niwe huru na niweze kuconnect na mimi mwenyewe, ni kitu ambacho nakipenda kutoka rohoni na I feel kwasababu nakipenda, ndio maana nakiweza kukifanya,” amesisitiza.

Usikilize wimbo wake Nana hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents