Tragedy

#GazaUnderAttack: Fahamu kwanini Israel na Palestina zinagombana juu ya Gaza

Kama ulikuwa na hamu ya kufahamu kwa maelezo rahisi na ya kueleweka ya kisa cha ugomvi wa Israel na Palestina uliodumu kwa miaka mingi na sasa ukatili ukiendelea huko Gaza, makala hii itakupa mwanga.

gaza9
Wapalestina wakiwa wamejihifadhi kwenye shule baada ya kukimbia makazi yao kufuatia mashambulio ya anga na ardhini ya Israel yanayoendelea kwenye ukanda wa Gaza

Waisrael na Waarabu wamekuwa wakiligombania eneo la Gaza kwa miongo mingi. Hiyo ni sehemu ya ugomvi mkubwa wa Israel ya Waarabu. Baada ya vita vikuu vya pili na kukatokea mauaji (Holocaust) ambapo wayahudi milioni sita waliuawa, Wayahudi zaidi waliitaka nchi yao. Walipewa eneo kubwa la Palestina, ambalo walilichukulia kama nyumbani kwao lakini Waarabu waliokuwa wakiishi hapo tayari pamoja na nchi jirani walihisi kuwa hiyo haikuwa sawa na hawakuikubali nchi mpya.

gaza1
Amka Twende: Wazee wa Palestina wakisaidiana kuokoa maisha yao

Mwaka 1948, pande hizo mbili ziliingia vitani. Vita ilipoisha, Gaza ikashikiliwa na Misri na eneo jingine la West Bank, likashikiliwa na Jordan. Maeneo hayo yalikaliwa na maelfu ya wapalestina waliokimbia eneo ambalo sasa ni nyumbani kwa wayahudi yaani Israel.

gaza2
Si Shwari tena: Mamia ya Wapalestina wanakimbia nyumba zao kuhofia maisha yao

Kutambulika kwa Israel

Lakini wakati huo, mwaka 1967, baada ya vita nyingine, Israel ikayashikilia maeneo haya ya Palestina, na majeshi ya Israel yakakaa hapo kwa miaka. Waisrael walitumai kuwa wanaweza kubadilishana eneo hilo walilolichukua na nchi za Kiarabu zitambue uwepo wa Israel na kumaliza vita.

Hatimaye, Israel iliondoka Gaza mwaka 2005 lakini baadaye tena, kundi liitwalo Hamas (chama cha kiisalamu cha Palestina) lilishinda uchaguzi na kuchukua udhibiti katika eneo hilo. Sehemu nyingi duniani inalitambua Hamas kama kundi la kigaidi. Kundi hilo Lilikataa kuitambua Israel kama nchini na linataka Wapalestina waweze kurudi katika makazi yao ya zamani na litafanya kila njia kufanikisha lengo lake hilo.

gaza3
Nyumba nyingi za Gaza zimebolewa na mashabulizi ya anga kutoka Israel

Tangu hapo, Israel imeishikilia Gaza kwa kuweka vizuizi, ikiwa na maana kuwa inashikilia mipaka yake na inasimamia nani anaweza kuingia au kutoka.

Maisha ya Gaza

gaza4
Tusaidieni? Mwanamke akilia kwa uchungu kutokana na hali ilivyo Gaza

Maisha ya Wapalestina takriban milioni 1.5 wanaoishi kwenye ukanda wa Gaza ni mabaya. Israel inashikilia fukwe zake na sehemu za kutoka na kuingia ndani ya Israel. Kuna njia nyingine ya kuingia kupitia Misri. Hakuna uwanja wa ndege unaotumika. Kwakuwa kuingia kumezuiliwa, hakuna bidhaa nyingi zinazoingia Gaza. Chakula kinaruhusiwa kuingia, lakini mashirika ya misaada yanadai kuwa familia hazili nyama ya kutosha ama mboga za majani au matunda kama walivyokuwa wamezoea. Huko mara nyingi umeme umekuwa ukikatwa. Watu wengi hawana ajira kwasababu wafanyabiashara hawana uwezo wa kutoa bidhaa nje ya Gaza ili kuuza na watu hawana fedha za kununua vitu.

Wakimbizi wa Palestina

gaza5
Familia nyingi zimekimbia makazi yao

Wakati wa vita vya mwaka 1948 na 1967 mamia kwa maelfu ya Wapalestina waliondoka, au waliondolewa kwa nguvu kwenye nyumba zao na kukimbilia katika nchi jirani na hivyo kugeuka wakimbizi. Zaidi ya Wapalestina milioni 4.6 ni wakimbizi na ndugu zao wanaishi kwenye makambi huko West Bank, Gaza, Syria, Jordan na Lebanon. Hupata msaada kutoka Umoja wa Mataifa.

Ukatili katika Gaza

gaza7
Tumekata tamaa

Ingawa Wapalestina hawana jeshi lolote, maroketi hurushwa mara kwa mara kutoka Gaza kwenda Israel. Waisrael wanaoishi kwenye miji iliyopo mpakani wamejikuta wakizoea kuishi maisha ya kushambuliwa na roketi hizo. Mwaka 2008, Israel ilituma wanajeshi kwenda Gaza. Takriban watu 1,300, wengi wao wakiwa raia wa kawaida waliuawa huko Gaza kabla ya mapatano ya kusitisha vita; wanajeshi 13 wa Israeli nao waliuawa.

gaza8
Mtoto aliyepigwa na bomu akiwa amebebwa

Mwaka 2012, takriban Wapalestina 167 na waisraeli waliuawa wakati wa operesheni ya Israel. Baada ya siku nane palipatikana mapato ya kusitisha mapigano na pande zote mbili kukubali kutofanya mashambulio.

gaza10
Shule zinatumika kama sehemu ya kujihifadhi kwa muda kufuatia mashambulio ya Israel kwenye ukanda wa Gaza

Na hivi karibuni, July 2014, mamlaka za Palestina zimedai kuwa zaidi ya watu 300 wameuawa kutokana na mashambulio ya anga ya Israel na wengi wamejeruhiwa. Israel inasema zaidi roketi 1,100 zilirushwa kutoka Gaza, na kujeruhi vibaya takriban Waisrael ‘wanne na Muisraeli mmoja kuuawa’ na hivyo mashambulio hayo ni ya kulipiza kisasi.

https://www.youtube.com/watch?v=qmJ7heWCX-0

Baada ya kuanzisha mashambulizi ya ardhini, July 17, Israel ilisababisha idadi ya vifo kuwa zaidi ya 300 na kuharibu nyumba, hospitali na mabomba ya maji huku watu zaidi 50,000 wakikimbia nyumba zao. “Operation Protective Edge” imeifanya Palestina kuwa jehanamu ya duniani.

gaza11
Mtoto aliyepigwa na bomu

Mchakato wa kutafuta amani

Nchi mbalimbali hasa Marekani, zimejitahidi kutafuta suluhu kati ya Waarabu na Waisrael lakini hadi sasa hakuna kilichofanikiwa. Wengi wanataka Gaza na West Bank kuwa kwenye nchi mpya, Palestina. Israel haiwezi kukubali labda kama ikihisi ina amani – na kama Hamas ikikubali uwepo wa Israel.

Vyanzo: BBC News, Aljazeera, Twitter

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents