Habari

Gardner G Habash Atua Rasmi Times FM


Mtangazaji na mjasiriamali Gardner G. Habash jana ametambulishwa rasmi katika kituo cha Radio Times FM na kumaliza uvumi uliokuwa umeanza kuenea wa wapi Gardner anaelekea, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili baada ya kujiuzuru kazi ya utangazaji katika msimu wa mwisho wa mwaka wa 2010.

Hafla ya kumtambulisha mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Radio ya Clouds FM kwa waandishi wa habari ilifanyika katika kiota cha chakula, vinywaji na burudani ya luninga za michezo City Sports Lounge ambapo Mtangzaji Scholastica Mazura ambaye ndiye mhariri mkuu wa habari katika Radio Times Fm alimtambulisha.

Gardner atakuwa akitangaza kipindi kinachoitwa Maskani ambacho kitakuwa kinaruka hewani kuanzia majira ya saa kumi alasiri mpaka saa moja usiku kuanzia siku ya Jumatatu ya Tarehe 3 Mwezi wa Tisa.
Bongo5 inapenda kumpongeza bwana G Habash kuendeleza libeneke.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents