Burudani

Galaxy: Remix ya ‘Top In My Heart’ nimemshirikisha msanii wa Nigeria

Galaxy amedai kuwa anatarajia kuachia remix ya wimbo wa ‘Top In My Heart’ aliomshirikisha msanii wa Nigeria.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5, kwenye remix hiyo amebadilisha kuanzia beat pamoja na kuchanganya baadhi ya ladha nyingine za muziki kutoka Afrika Magharibi.

“Remix ya ‘Top In My Heart’ inakuja ambayo nimemshirikisha msanii kutoka Nigeria. Natarajia itafanya vizuri kwa kuwa beat ni tofauti kabisa na nimechanganya ladha tofauti za magharibi na Bongo. Kwa sasa ngoma imekamilika ila tunafanya mpango wa video ambapo muda si mrefu huyo msanii atatua Bongo kwaajili ya media tour pamoja na kufanya hiyo video ili tuweze kuiachia,” amesema Galaxy.

Msanii huyo ameongeza kuwa baada ya kuachia video ya wimbo huo atasafiri kuelekea nchini Nigeria kwa ajili ya kutafuta connection zaidi za muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents