Burudani

Galaxy: Kiki hazimsaidii msanii, muziki mzuri ndio kila kitu

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Tam Tam’ huku sasa akiwa na wimbo, ‘Top In My Heart’, Galaxy amedai kuwa kiki haziwezi kumsaidia msanii bali muziki mzuri.

Galaxy amesema kiki hazisaidii ‘kuboost’ muziki wa msanii, ila msanii mwenyewe anapohakikisha anaachia nyimbo nzuri na kuonesha uwezo wake.

“Situmi kiki yeyote kuboost muziki wangu au kutaka nifahamike kwa kupitia kiki,” amesema.

“Mimi naona mwisho wake ni mbaya kwakuwa wasanii wengi nawaona wanatafuta kiki zingine zisizokuwa na maana halafu baadaye wanakuja kudhalilika tu katika jamii, kitu ambacho naona wanakosea sana. Ila msanii anapoachia nyimbo kali na nzuri hicho ndio kitu ambacho kitaonesha uwezo wako kwa mashabiki kuweza kukubalika,” muimbaji huyo ameiambia Bongo5.

“Mimi nawashauri bora waongeze juhudi kuboresha muziki ili uwe mzuri maana kwa upande wa kiki naona wanapoteza muda mwingi na mwisho wa siku hakuna nyimbo za maana wanaimba na hazikai sokoni kwa muda mrefu kwakuwa hakuna muziki mzuri,” ameongeza.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents