Habari

Gadner G Habash ahamia EFM, ataendesha show ya jioni ‘Ubaoni’

Gadner G Habash amejiunga na kituo cha redio cha EFM 93.7 Dar es Salaam.

Producer-Lamar-na-Gagna-G
Gadner (kulia) akiwa na Lamar kwenye uzinduzi wa video za Profesa Jay hivi karibuni

Kabla ya hapo, mtangazaji huyo mkongwe alikuwa akiendesha kipindi cha jioni, Maskani cha Times FM.

“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu,” afisa habari wa kituo hicho Kanky Mwaigomole aliwaambia waandishi wa habari.

Gadner ni miongoni mwa watangazaji wanaoheshimika zaidi nchini na alijizolea umaarufu zaidi kupitia Clouds FM aliyoitumikia kwa miaka mingi kabla ya kuondoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents